NAFASI MPYA ZA AJIRA KAHAMA MUNICIPAL COUNCIL 2025

Ajira Mpya Kahama Municipal Council Mei 2025

Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imetangaza nafasi mpya za ajira kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kufuatia kibali cha ajira kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichotolewa tarehe 29 Aprili 2025. Watanzania wenye sifa wanakaribishwa kutuma maombi kuanzia Mei 14, 2025.

Nafasi Zinazotangazwa:

1. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II – Nafasi 04

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya kidato cha nne au sita
  • Stashahada (NTA Level 6) katika:
    • Utunzaji wa Kumbukumbu
    • Urasimu Ramani (Cartography)
    • Geo-Informatics
    • Sheria
    • Kumbukumbu za Afya
  • Ujuzi wa matumizi ya kompyuta kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali

Majukumu:

  • Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka
  • Kusambaza na kupokea majalada
  • Kutafuta na kurudisha kumbukumbu
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada

Mshahara: Kwa mujibu wa ngazi ya serikali ya TGS C1

2. Dereva Daraja II – Nafasi 03

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya kidato cha nne au sita (kuanzia daraja la nne)
  • Mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari kutoka VETA, NIT au chuo kinachotambuliwa na serikali
  • Leseni ya daraja C au E
  • Awe mwadilifu na hajawahi kutiwa hatiani

Majukumu:

  • Kukagua usalama wa gari
  • Kuwasafirisha watumishi
  • Kusambaza nyaraka
  • Kuhifadhi taarifa za safari
  • Kufanya usafi wa gari

Mshahara: Kwa mujibu wa ngazi ya serikali ya TGS B1

Masharti ya Jumla kwa Waombaji Wote:

  • Awe Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45
  • Ambatanisha nakala ya cheti cha kuzaliwa
  • Ambatanisha C.V yenye taarifa binafsi na namba za simu
  • Ambatanisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na wakili au Kamishna wa viapo
  • Vyeti vya nje ya nchi lazima vifanyiwe ulinganishi na TCU au NACTE
  • Ambatanisha picha moja ya “passport size” ya hivi karibuni
  • Maombi yaandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza na yasainiwe

Jinsi ya Kutuma Maombi:

Tuma maombi kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira kwa anuani:
🔗 https://portal.ajira.go.tz

Anuani ya barua:
Mkurugenzi wa Manispaa,
Barabara ya Boma,
S.L.P 472,
KAHAMA – Shinyanga.

⚠️ Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatazingatiwa.


🗓 Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 27 Mei, 2025. Usikose fursa hii ya kujiunga na Manispaa ya Kahama.

Romann Fitz

My name is Romann and this is my blog. I started this blog as a side project back in 2021, My goal is to provide all Latest Education and Admission Portal: University portal and admission requirements. Vacancies, Internship Updates in Africa

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post