Ratiba Kamili ya Muungano Cup 2025: Robo Fainali Hadi Fainali
Ratiba ya Kombe la Muungano 2025 Yatangazwa Rasmi
Michuano ya Kombe la Muungano kwa mwaka 2025 inatarajiwa kuanza rasmi Jumatano ya tarehe 23 Aprili katika Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar. Mashindano haya yamekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka Tanzania Bara na Visiwani, yakileta ushindani mkubwa kati ya klabu bora kutoka pande zote mbili.
Ratiba ya Kombe la Muungano 2025 kuanzia Robo Fainali hadi Fainali:
Tarehe | Saa | Mechi | Hatua |
---|---|---|---|
24 Aprili 2025 | 14:15 | Zimamoto SC vs Coastal Union | Robo Fainali |
24 Aprili 2025 | 16:15 | KMKM SC vs Azam FC | Robo Fainali |
25 Aprili 2025 | 20:15 | KVZ FC vs Yanga SC | Robo Fainali |
27 Aprili 2025 | 20:15 | JKU/Singida BS vs KMKM/Azam FC | Nusu Fainali |
28 Aprili 2025 | 20:15 | Zimamoto/Coastal Union vs KVZ/Yanga | Nusu Fainali |
30 Aprili 2025 | 20:15 | Washindi wa Nusu Fainali | Fainali |
Ratiba ya Robo Fainali
Robo fainali za Kombe la Muungano mwaka huu zitachezwa kwa siku tatu kuanzia Aprili 23 hadi Aprili 25, zikiwa na mechi kali zinazotarajiwa kuamua timu zitakazoingia nusu fainali. Hii hapa ni ratiba kamili:
23 Aprili 2025
Saa 10:15 Jioni: JKU SC dhidi ya Singida Black Stars
24 Aprili 2025
Saa 8:15 Mchana: Zimamoto SC dhidi ya Coastal Union
Saa 10:15 Jioni: KMKM SC dhidi ya Azam FC
25 Aprili 2025
Saa 2:15 Usiku: KVZ FC dhidi ya Yanga SC
Soma: Viingilio vya Mechi ya Simba vs Stellenbosch Aprili 20
Ratiba ya Nusu Fainali
Nusu fainali zitaendelea siku mbili baada ya kumalizika kwa robo fainali, ambapo timu zitakazoshinda zitachuana kutafuta nafasi ya kufika fainali:
27 Aprili 2025
Saa 2:15 Usiku: Mshindi kati ya JKU SC na Singida Black Stars atakutana na mshindi kati ya KMKM SC na Azam FC
28 Aprili 2025
Saa 2:15 Usiku: Mshindi kati ya Zimamoto SC na Coastal Union atakutana na mshindi kati ya KVZ FC na Yanga SC
Fainali ya Kombe la Muungano 2025
Mechi ya fainali ya Kombe la Muungano itafanyika Aprili 30, 2025 kuanzia saa 2:15 usiku. Fainali hii itawakutanisha washindi wa nusu fainali mbili na mshindi atatajwa kuwa bingwa wa Kombe la Muungano kwa mwaka huu.
Mashindano haya si tu yanatoa burudani kwa mashabiki, bali pia yanazidi kuimarisha ushirikiano na mshikamano wa michezo kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.